Customer Service Week 2016

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhayay (katikati) katika picha ya pamoja na maofisa ya benki ya CRDB tawi laMlimani City ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Watejana (wa tano kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango.


Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhayay (kushoto) akiwaongoza wateja wa Benki hiyo tawi la Mlimani City kunyanyua juu glasi zilizokuwa na kinywaji cha shampeni.Mteja wa muda mrefu akiwa anakata Keki ya maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja ikiwa na kauli mbiu ya Tunakusikiliza, karibu tukuhudumie.


Meneja waenki ya CRDB Tawi la Tegeta Kibo Complex, Richard Mkakala akimlisha keki mteja wa muda mrefu wa tawi la Tegeta ikiwa ni kuadhisha wiki ya huduma kwa wateja.


Mkurugenzi wa Nemarty Limited, Neema Lyimo akikata keki kwa niaba ya wateja wa tawi la Benki ya CRDB tawi la Water Front wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Water Front.


Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.


Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo akizungumza na Wateja pamoja na Wafanyakazi wa Benki hiyo ikiwa ni muendelezo wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba 3 Duniani kote ambapo wateja wa CRDB wataendelea kujivunia mafanikio ya Benki hiyo.


Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo akishirikiana na mmiliki wa Kampuni ya Easy Connections, Justus Bashara wakati wa hafla hiyo.


Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay alipotembelea tawi la Tegeta Kibo Complex na kukata keki pamoja nao katika wiki ya huduma kwa wateja. Pembeni yake kulia ni mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja Bi. Tully Esther Mwambapa.


Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Tegeta Kibo Complex wakiwa katika picha ya Pamoja katika wiki ya huduma kwa wateja.


Meneja wa Tawi letu la Gairo akiwatwisha maji akina mama baada ya uzinduzi wa kisima kilichochimbwa na Benki ya CRDB tawi la Gairo katika wiki ya huduma kwa wateja


Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Tegeta Kibo Complex, Richard Mkakala akisaidiana na wateja wa benki ya CRDB tawi la Tegeta kukata keki kwaajili ya kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja.


Misaada kwa jamii zilizosahaulika ni sehemu ya maadhimisho yetu ya wiki ya huduma kwa wateja


Wiki ya Huduma kwa wateja Mbeya, Karibu Tukuhudumie.(function($){ $(document).on('ready', function() { }); })(jQuery);