“Benki ya CRDB yaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2016”

Dar es Salaam Tanzania, Octoba 3, 2016 – Ikiwa ni mwendelezo wa jitihada zake za kuboresha huduma kwa wateja wake, Benki ya CRDB inakuletea “Wiki ya Huduma kwa Wateja” kuanzia Jumatatu tarehe 3 hadi 8 mwezi Octoba, 2016.


Wiki hii ambayo mwaka huu itakuwa na kauli mbiu ya “Tunasikiliza karibu tukuhudumie” ni maalum kwa ajili ya kuwakaribisha wateja wa Benki ya CRDB kufurahia bidhaa na huduma bunifu zinazotolewa na Benki ya CRDB ikiwa ni pamoja na kutambua na kuthamini mchango wa wateja wake katika maendeleo ya Benki.

Benki ya CRDB inatambua na kuthamini ukweli kuwa wateja wake ndio chanzo cha kila jema linalotokea kwa Benki ya CRDB”. Katika wiki hii maalum kwa ajili wateja, Benki ya CRDB inawakaribisha wateja wake wote kwa kipekee kabisa kutembelea matawi yake ili kupata huduma bora zaidi na kutoa maoni au ushauri ili kuiwezesha Benki kutoa huduma na bidhaa bora zaidi zitakazo fikia na kuzidi matarajio ya wateja.

Ikiwa ni Benki inayoongozwa na kauli mbiu isemayo “Benki inayomsikiliza mteja”, Benki ya CRDB inaamini katika kusikiliza mahitaji, maoni na ushauri wa wateja wake ili kuboresha huduma na bidhaa.

Pamoja na kupata maoni au ushauri wa wateja juu ya huduma na bidhaa za Benki ya CRDB, uongozi wa juu wa Benki ya CRDB ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Charles Kimei na wakurugenzi wa idara mbalimbali, watakuwepo kwenye matawi kwa ajili ya kutoa huduma na kukutana na wateja ana kwa ana.

Kama hilo halitoshi, Benki ya CRDB pia itatumia wiki hii kutoa misaada mbalimbali kwa jamii na kutembelea maeneo yenye mahitaji ikiwemo mahospitali, mashule na vituo vya watoto yatima.

Benki ya CRDB inachukua fursa hii kuwakaribisha wateja wake wote kutembelea matawi ya Benki ya CRDB pale walipo katika kipindi hiki cha Wiki ya Huduma kwa Wateja.

-MWISHO-

Kuhusu Benki ya CRDB Benki ya CRDB ilianzishwa mwaka 1996 na imeendelea kukua zaidi hadi kufikia kuwa benki inayoaminika, chaguo la kwanza la mteja na kuongoza kwa ubanifu katika soko. Benki ya CRDB imekuwa ikirekodi ongezeko la faida kila mwaka tokea ilipoanzishwa na imekuwa ikilipa gawio kila mwaka kwa wanahisa wake. Benki ilipiga hatua muhimu hivi karibuni baada ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kuanzisha kampuni tanzu ya CDRB Burundi.

Benki ya CRDB inatoa huduma mbalimbali kwa wateja wakubwa, wakati na wadogo kupitia matawi zaidi ya 200, Matawi yanayotembea 12, Mashine za kutolea hela zaidi ya 500, Mashine za kuweka hela 15, vifaa vya manunuzi (PoS) zaidi ya 1,000 na Mawakala wa FahariHuduma zaidi ya 2000. Pia Benki ya CDRB inatoa huduma ya kibenki kupitia mtandao “Internet banking” na huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimBanking.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Jina Namba ya Simu Barua Pepe
Tully Esther Mwambapa +255 769 200 600

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

(function($){ $(document).on('ready', function() { }); })(jQuery);