Benki ya CRDB yawazawadia washindi wa kampeni ya “Shinda na TemboCard”

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akitoa hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni ya "Shinda na TemboCard"
Dar Es Salaam Tanzania, Juni 20, 2016– Benki ya CRDB imetoa zawadi za kwanza kwa washindi wa kampeni yake ya “Shinda na TemboCard” katika hafla fupi iliyo fanyika katika hoteli ya Ramada Encore iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Akizungumza katika hafla hiyo ya utoaji zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei alisema, “leo tupo hapa ili kutoa zawadi kwa washindi wetu wa shindano hili kwa mwezi wa Mei, 2016”.


“Akielezea dhumuni la kuendesha kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei alisema Benki ya CRDB imeamua kuanzisha kampeni hiyo ili kuwakumbusha wateja wake na watanzania kwa ujumla umuhimu wa kutumia njia hiyo mbadala ya kutolea huduma ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka zaidi. “Tunataka kuwavutia wateja wetu kuiamini na kutumia zaidi huduma hii ya malipo kupitia kadi kwani ni rahisi, nafuu na salama pia haimhitaji mteja kutembea na kiasi kikubwa cha fedha ili kufanya manunuzi” alisema Dkt.Kimei.

Mjumbe wa Bodi ya CRDB Mr.Ally Laay pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei wakimkabidhi mfano wa tiketi mshindi wa kwanza wa kampeni ya "Shinda na TemboCard" Mr.Ismail O. Jimroger aliyejishindia mapumziko na familia kwenda Dubai


“Kwa mara ya kwanza Benki ya CRDB ilizindua huduma ya TemboCard mwaka 2002, ikilenga kuwapa wateja wake urahisi na unafuu wa upatikanaji wa huduma popote walipo kupitia kadi hizo za TemboCard. Uzinduzi wa huduma hiyo ya TemboCard pia ulilenga kupunguza hatari ya wateja kutembea na fedha nyingi kwa ajili ya kufanya manunuzi ambapo Benki ya CRDB ilizindua mfumo wa malipo kwa kupitia vifaa maalum vya manunuzi (Point of Sales) ambao umefanikiwa kuwawezesha wateja kupata huduma kwa urahisi na unafuu. Vifaa hivyo vya malipo ambavyo vimesambazwa katika biashara na taasisi mbalimbali, vimefanikiwa kusaidia ukusanyaji wa mapato katika biashara na taasisi hizo kwa kiasi kikubwa. Mpaka sasa Benki ya CRDB imefanikiwa kutoa jumla ya TemboCard 1,600,000 pamoja kusambaza jumla ya vifaa vya manunuzi 1,500 kwa biashara na taasisi mbalimbali nchi nzima, kama supamaketi, maduka ya rejareja, hospitali, hoteli, mbuga za wanyama pamoja na taasisi nyingine mbalimbali binafsi na za serikali.


Bi.Juliana J. Utamwa ambaye pia alijishindia mapumziko na familia kwenda Dubai kwa upande wa wafanyakazi wa Benki ya CRDB

Dkt. Kimei alisema kampeni hiyo imeanza kuzaa matunda ikiwa ni mwezi mmoja tu tokea kuanzishwa kwake. Jumla ya miamala katika PoS imeongezeka hadi kufikia 193,605 kwa mwezi Mei kutoka 162,181 mwezi wa Aprili. Wakati thamani ya miamala kupitia PoS imeongezeka kutoka shilingi bilioni 11.56 mwezi Aprili hadi kufikia shilingi bilioni 14.89 mwezi Mei. Kwa upande wa manunuzi kupitia mtandaoni (Online Purchase) miamala imeongezeka kutoka 5,937 mwezi Aprili hadi kufikia 6,948 mwezi Mei. Ongezeko hili limechangia kukua kwa thamani ya miamala kupitia PoS kutoka shilingi milioni 638.43 mwezi Aprili hadi kufikia shilingi bilioni 715.56 mwezi Mei.


Jumla ya washindi watano wa kampeni ya “Shinda na TemboCard” kwa mwezi mei walitangazwa ambapo mshindi wa kwanza alikuwa Bw. Ismail Omary Jimroger mshindi ambaye alijishindia safari ya kifahari yeye pamoja na familia yake kwenda Dubai. Washindi wengine katika kampeni hiyo walikuwa ni Bi. Zubeda Ahmed Chande aliyejishindia zawadi ya Laptop aina ya Mac Book Pro, Ndg. Nam Jin aliyejishindia iPad, Ndg. Dereck Donald Mazige aliyejishindia simu ya kisasa aina ya iPhone 6 na Ndg. Belinda Deogratius Msaki aliyejishindia simu aina ya Samsung J5.

Mkurugenzi wa Maisha Finance Ltd, Mr.Deus Manyenye aliyeibuka mshindi kwa upande wa FahariHuduma Wakala akikabidhiwa Zawadi yake ya Laptop (Mac Book Air)

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo Bw. Ismaili Omary Jimroger alisema, “kwanza kabisa siwezi kuamini kwamba nimeshinda safari ya kwenda Dubai pamoja na familia yangu, nina furaha kupita kiasi, mimi nimtumiaji mzuri sana wa huduma zinazopatikana kupitia TemboCard, mara nyingi huwa natumia TemboCard yangu kulipia manunuzi ya nyumbani, kulipia mafuta kwenye vituo vya kujazia mafuta, pamoja na kufanya manunuzi kupitia mtandao, siku zote imekuwa ikinirahisishia kupata huduma pale Nilipo, nadhani mazoea haya na kufanya miamala mingi ndiyo iliyopelekea leo hii mimi kushinda”,”


Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Dkt. Charles Kimei aliwapongeza washindi wote walioibuka kidedea katika shindano hilo. Dkt. Kimei pia aliwasihi wateja wengine wa Benki hiyo kuendelea kushiriki katika Shindano hilo, na kusema kuwa, shindano hilo ni kwa wateja wote wa Benki ya CRDB na mshindi atakuwa ni mteja atayefanikiwa kufanya miamala mingi zaidi ya manunuzi kupitia kadi yake ya TemboCard Visa au MasterCard kwa mwezi husika. Dkt. Kimei alisema pia kuwa shindano hilo ni rahisi sana kwani wateja wanachotakiwa kufanya ni kutumia kadi zao na kufanya manunuzi mara nyingi zaidi na mtumiaji mwenye miamala mingi zaidi ndio ataibuka Mshindi. “Mshindi ni yule atakayekuwa amefanya miamala mingi zaidi ya manunuzi kupitia kadi yake ya TemboCard Visa au MasterCard katika mwezi husika, iwe ni malipo ya bidhaa au huduma kupitia vifaa maalumu vya manunuzi (Point of Sales), manunuzi ya bidhaa mtandaoni (online purchases) kupitia kadi au kutoa pesa na kufanya malipo kupitia kadi kwa mawakala wa FahariHuduma” alifafanua Dkt. Kimei.

Mama yake na Zubeda Ahmed Chande akipokea Laptop (Mac Book Air) kwa niaba ya binti yake

Urahisi, usalama na unafuu wa huduma ya TemboCard unawawezesha wateja wengi wa Benki ya CRDB kufanya malipo kwa ajili ya bidhaa na huduma mbalimbali bila kuhitaji fedha taslimu. Akihutubia wageni waalikwa katika hafla hiyo ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya “Shinda na TemboCard”, Dkt. Kimei alisema kuwa ingawa huduma ya malipo kupitia TemboCard imeonesha mafanikio mazuri sokoni bado juhudi zaidi zinahitajika ili kuwavuta wateja wengi zaidi kutumia huduma hiyo mbadala ya malipo.


Dkt. Kimei pia aliwasisitiza wateja wa Benki hiyo kuendelea kutumia mawakala wa FuhariHuduma kwani kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kusogeza huduma za Benki hiyo karibu zaidi na wateja. “Mbali na kutizama miamala ya malipo kupitia vifaa vya manunuzi (Point of Sales), miamala ya manunuzi ya bidhaa mtandaoni (online purchases), vilevile kampeni yetu itajumuisha miamala yote ya kadi kupitia kwa mawakala wetu wa FahariHuduma ili kuwapa wateja chachu ya kuendelea kufurahia huduma kupitia mfumo huu maalum wa utoaji huduma” alisema Dkt. Kimei.

Mr.Nam Jin (katikati) aliyeibuka mshindi wa tatu akipokea zawadi yake ya I Pad.

Mawakala wa FahariHuduma hutoa huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo ikiwemo kuweka na kutoa fedha kwenye akaunti za wateja, kutuma fedha kwa watu walio na wasio na akaunti za Benki, kupokea fedha, kupokea marejesho ya mikopo, kulipia Ankara mbalimbali, kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti nyingine ndani ya benki ya CRDB, kuangalia salio na kuchukua kadi za Benki ya CRDB.

Barbara Hassan, mtangazaji wa Power Breakfast ya Clouds FM akikabidhiwa zawadi yake ya simu aina ya I Phone 6 baada ya kuibuka mshindi katika kipengele cha waandishi wa habari.

Akiongea katika hafla hiyo Ndg. Ally Laay ambaye alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni hiyo ya “Shinda na TemboCard” akimuwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, alisema kuwa Bodi ya Benki Ya CRDB inafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kuwa benki ya CRDB inakuwa na njia mbadala za kutolea huduma ili kuwapa wateja wake wasaa wa kupata huduma kwa muda na mahali watakapo. “Lengo letu ni kuhakikisha kuwa zile zama za kila mtu kuja kwenye tawi la benki ili kuhudumiwa zinakuwa ni historia kwani anaweza kupata huduma zetu popote alipo” alisema Ndg. Laay ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugunzi Benki hiyo. Ndg. Laay alisema huduma za malipo kupitia kadi za TemboCard, ni moja ya huduma ambazo zimeleta mapinduzi makubwa sana katika sekta ya mabenki nchini, hususani katika kuwaondolea wateja ulazima wa kutembea na kiasi kikubwa cha fedha na hivyo kuhatarisha maisha yao.

Mkurugenzi wa tawi la Lumumba, Bi. Pendo Assey (katikati) akiwa na mshindi wa tatu kwa upande wa wafanyakazi, Bi.Mwanahamisi Mohammed aliyejishindia I Pad. Wengine ni Mr.Ally Laay, Dr.Charles Kimei na Marinatha Lyimo Ndel(kulia).

Dkt. Kimei alimalizia kwa kuwashukuru wateja wa Benki hiyo kwa kuifanya kuwa Benki nambari moja na bora zaidi, huku akisema kuwa wateja wa Benki hiyo wamekuwa na mchango mkubwa sana katika ukuaji wa Benki ya CRDB. Huku akiwakumbusha kuwa huo sio mwisho wa kampeni hiyo bali ndio mwanzo kwani kuna miezi mitano zaidi ambapo washindi wengine watakuwa wakitangazwa kila mwezi.

Belinda Deogratius Msaki akiwa ameshika simu aina ya Samsung J5 aliyozawadiwa kwa kuibuka mshindi wa tano katika kampeni ya mwezi Mei.
 

-MWISHO-

Kuhusu Benki ya CRDB

Benki ya CRDB ilianzishwa mwaka 1996 na imeendelea kukua zaidi hadi kufikia kuwa benki inayoaminika, chaguo la kwanza la mteja na kuongoza kwa ubanifu katika soko. Benki ya CRDB imekuwa ikirekodi ongezeko la faida kila mwaka tokea ilipoanzishwa na imekuwa ikilipa gawio kila mwaka kwa wanahisa wake. Benki ilipiga hatua muhimu hivi karibuni baada ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kuanzisha kampuni tanzu ya CDRB Burundi.

Benki ya CRDB inatoa huduma mbalimbali kwa wateja wakubwa, wakati na wadogo kupitia matawi zaidi ya 198, Matawi yanayo tembea 12, Mashine za kutolea hela zaidi ya 461, Mashine za kuweka hela 15, vifaa vya manunuzi (PoS) zaidi ya 1,500 na Mawakala wa FahariHuduma zaidi ya 1,769. Pia Benki ya CDRB inatoa huduma ya kibenki kupitia mtandao “Internet banking” na huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimBanking.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Jina Namba ya Simu Barua Pepe
Tully Esther Mwambapa +255 769 200 600

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Godwin Semunyu +254 784 002 020 This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

(function($){ $(document).on('ready', function() { }); })(jQuery);