Benki ya CRDB yazindua kampeni ya “Shinda na TemboCard” kwa ajili ya wateja wake

Dar Es Salaam Tanzania, Aprili 28, 2016 – Benki ya CRDB leo imezindua kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma zake ya kibenki kupitia kadi maalum za TemboCard Visa au MasterCard ambayo inawapa wateja wa benki hiyo nafasi ya kujishindia Safari ya kwenda Dubai pamoja na familia zao. Uzinduzi huo ambao ulifanyika katika makao makuu ya Benki hiyo yaliyopo mtaa wa Azikiwe katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi pamoja na baadhi ya wateja wa Benki hiyo.


“Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama “Shinda na TemboCard”, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei alisema Benki ya CRDB imeamua kuanzisha kampeni hii ili kuwakumbusha wateja wake na watanzania kwa ujumla umuhimu wa kutumia njia hiyo mbadala ya kutolea huduma ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka zaidi. “Tunataka kuwavutia wateja wetu kuamini na kutumia zaidi huduma hii ya malipo kupitia kadi kwani ni rahisi, nafuu na salama kwani haimhitaji mteja kutembea na kiasi kikubwa cha fedha ili kufanya manunuzi” alisema Dkt.Kimei.

“Kampeni ya “Shinda na TemboCard”, inatarajiwa kuwapa nafasi wateja wa Benki ya CRDB kujishindia nafasi ya kusafiri pamoja na familia zao ambapo kila mwezi mshindi mmoja atapata nafasi ya kutembelea mbuga za wanyama zaSerengeti, Mikumi, Ngorongoro, Selous, na Manyara au mji wa kihistoria wa Zanzibar, na Mshindi atakayekuwa na miamala mingi zaidi mwisho wa kampeni kupata nafasi ya kwenda nchini Dubai au Afrika Kusini yeye pamoja na familia yake. Pamoja na zawadi hizo wateja wa Benki hiyo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine mbalimbali kama vile Tablets, iPads na Simu za mkononi (Smartphone) kila mwezi kwa muda wa miezi sita. Kila mwezi Benki hiyo itatoa zawadi kwa jumla ya wateja 20 ambao watakuwa wameibuka washindi katika kampeni hiyo maalum.

Akielezea namna ya kushiriki na jinsi mshindi atakavyopatikana, Dkt. Kimei alisema “Shindano hili ni kwa wateja wote wa Benki ya CRDB na mshindi atakuwa ni mteja atayefanikiwa kufanya miamala mingi zaidi ya manunuzi kupitia kadi yake ya TemboCard Visa au MasterCard kwa mwezi husika”. Dkt. Kimei alisema pia kuwa shindano hilo ni rahisi sana kwani wateja wanachotakiwa kufanya ni kutumia kadi zao na kufanya manunuzi mara nyingi zaidi na mtumiaji mwenye miamala mingi zaidi ndio ataibuka Mshindi. “Mshindi ni yule atakayekuwa amefanya miamala mingi zaidi ya manunuzi kupitia kadi yake ya TemboCard Visa au MasterCard katika mwezi husika, iwe ni malipo ya bidhaa au huduma kupitia vifaa maalumu vya manunuzi (Point of Sales), manunuzi ya bidhaa mtandaoni (online purchases) kupitia kadi au kutoa pesa na kufanya malipo kupitia kadi kwa mawakala wa FahariHuduma”.,” alifafanua Dkt. Kimei.

Kwa mara ya kwanza Benki ya CRDB ilizindua huduma ya TemboCard mwaka 2002, ikilenga kuwapa wateja wake urahisi na unafuu wa upatikanaji wa huduma popote walipo kupitia kadi hizo za TemboCard. Uzinduzi wa huduma hiyo ya TemboCard pia ulilenga kupunguza hatari ya wateja kutembea na fedha nyingi kwa ajili ya kufanya manunuzi ambapo Benki ya CRDB ilizindua mfumo wa malipo kwa kupitia vifaa maalum vya manunuzi (Point of Sales) ambao umefanikiwa kuwawezesha wateja kupata huduma kwa urahisi na unafuu. Vifaa hivyo vya malipo ambavyo vimesambazwa katika biashara na taasisi mbalimbali, vimefanikiwa kusaidia ukusanyaji wa mapato katika biashara na taasisi hizo kwa kiasi kikubwa. Mpaka kufikia mwezi Machi mwaka huu Benki ya CRDB imefanikiwa kusambaza jumla ya vifaa vya manunuzi 1,500 kwa biashara na taasisi mbalimbali nchi nzima, kama Supermarkets, maduka ya rejareja, hospitali, hoteli, mbuga za wanyama pamoja na taasisi nyingine mbalimbali binafsi na za serikali.

Ni miaka sasa 14 tokea kuanzishwa kwa huduma ya kadi ya TemboCard mapaka sasa Benki ya CRDB imefanikiwa kutoa jumla ya TemboCard 1,600,000 kwa wateja wake ambazo zimekuwa zikitumika kuchukua fedha katika mashine za ATM, malipo ya bidhaa na huduma kupitia vifaa vya manunuzi (Point of Sales) na pamoja na kufanya manunuzi mtandaoni (online purchase). Kadi hizi zimewavutia wateja wengi kutokakana na kutoa unafuu na urahisi wa kufanya malipo pasipo kutoa fedha taslimu kwenye matawi ya Benki au mashine za ATM. Vilevile, kadi hizi zimepunguza matukio ya wizi na ukabaji kwani watu wengi wameonyesha kuacha utamaduni wa kutembea na hela kwaajili ya kufanya malipo na kuvutiwa na mfumo huu mpya. Takwimu zinaonyesha zaidi ya nusu ya wateja wote wenye TemboCard wamekuwa wakitumia kadi zao kufanya malipo.,”

Urahisi, usalama na unafuu wa huduma ya TemboCard unawawezesha wateja wengi wa Benki ya CRDB kufanya malipo kwa ajili ya bidhaa na huduma mbalimbali bila kuhitaji fedha taslimu. Akihutubia wageni waalikwa katika hafla hiyo ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya “Shinda na TemboCard”, Dkt. Kimei alisema kuwa ingawa huduma ya malipo kupitia TemboCard imeonesha mafanikio mazuri sokoni bado juhudi zaidi zinahitajika ili kuwavuta wateja wengi zaidi kutumia huduma hiyo mbadala ya malipo.

Dkt. Kimei pia aliwasisitiza wateja wa Benki hiyo kuendelea kutumia mawakala wa FuhariHuduma kwani kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kusogeza huduma za Benki hiyo karibu zaidi na wateja. “Mbali na kutizama miamala ya malipo kupitia vifaa vya manunuzi (Point of Sales), miamala ya manunuzi ya bidhaa mtandaoni (online purchases), vilevile kampeni yetu itajumuisha miamala yote ya kadi kupitia kwa mawakala wetu wa FahariHuduma ili kuwapa wateja chachu ya kuendelea kufurahia huduma kupitia mfumo huu maalum wa utoaji huduma”, “ alisema Dkt. Kimei.

Mawakala wa FahariHuduma hutoa huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo ikiwemo kuweka na kutoa fedha kwenye akaunti za wateja, kutuma fedha kwa watu walio na wasio na akaunti za Benki, kupokea fedha, kupokea marejesho ya mikopo, kulipia Ankara mbalimbali, kuhamisha fedha kwenda kwenye akaunti nyingine ndani ya benki ya CRDB, kuangalia salio na kuchukua kadi za Benki ya CRDB.

Uzinduzi wa kampeni hii ya “Shinda na TemboCard”, unaleta chachu kwa watumiaji wa TemboCard na FahariHuduma kuendelea kufurahia huduma hizo huku wakijiweka katika nafasi nzuri ya kijishindia zawadi ya safari pamoja na familia zao.

Dkt. Kimei alitoa rai kwa wateja na watanzania wote kwa ujumla kuchangamkia ofa hii kwa kusema “Safari hii tumeamua kuwapa wateja wetu zawadi ya kusafiri na kufurahia pamoja na familia zao, hii ni zawadi kubwa na ya kipekee kabisa kwa wateja wetu. Ni rahisi sana, mteja anachotakiwa kufanya ni kuendelea kutumia kadi yake ya TemboCard kufanya malipo ya manunuzi” alisema Dkt.Kimei, huku akisisitiza kuwa mbali na zawadi hizo zitakazotolewa mwisho wa mwezi pia kutakuwa na zawadi za papo hapo kwa wateja watakaofanya manunuzi ya kuanzia kiasi cha shilingi elfu hamsini. Pia aliwatoa hofu wateja kuhusiana na makato kwani huduma ya malipo kupitia TemboCard hutolewa bure kwa wateja wote na hivyo basi kuwasihi wateja kujenga utamaduni wa kutumia kadi kufanya malipo kwani ni rahisi, salama na nafuu zaidi.

Dkt. Kimei alimalizia kwa kuwashukuru wateja wa Benki hiyo kwa kuifanya kuwa Benki nambari moja na bora zaidi nchini, huku akisema kuwa wateja wa Benki hiyo wamekuwa na mchango mkubwa sana katika ukuaji wa Benki ya CRDB. “Mwaka huu tunasherehekea miaka 20 tokea kuanzishwa kwetu ambapo tumeipa jina “Miaka 20 ya Ukuaji na Kuboresha Maisha”, tunajivunia sana mafanikio haya na tunawashukuru wateja wetu, kampeni hii ni sehumu pia ya shukrani kwa wateja wetu kwa kutuamini”. Dkt. Kimei pia aliwakaribisha wateja wengine ambao bado hawana akaunti Benki ya CRDB kutembelea katika matawi ya karibu na kuweza kufungua akaunti ambapo watapewa kadi ya TemboCard Visa au MasterCard bure zitakazowawezesha kufanya malipo na kuingia moja kwa moja katika shindano la “Shinda na TemboCard”..
 

-MWISHO-

Kuhusu Benki ya CRDB

Benki ya CRDB ilianzishwa mwaka 1996 na imeendelea kukua zaidi hadi kufikia kuwa benki inayoaminika, chaguo la kwanza la mteja na kuongoza kwa ubanifu katika soko. Benki ya CRDB imekuwa ikirekodi ongezeko la faida kila mwaka tokea ilipoanzishwa na imekuwa ikilipa gawio kila mwaka kwa wanahisa wake. Benki ilipiga hatua muhimu hivi karibuni baada ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kuanzisha kampuni tanzu ya CDRB Burundi.

Benki ya CRDB inatoa huduma mbalimbali kwa wateja wakubwa, wakati na wadogo kupitia matawi zaidi ya 198, Matawi yanayo tembea 12, Mashine za kutolea hela zaidi ya 461, Mashine za kuweka hela 15, vifaa vya manunuzi (PoS) zaidi ya 1,500 na Mawakala wa FahariHuduma zaidi ya 1,769. Pia Benki ya CDRB inatoa huduma ya kibenki kupitia mtandao “Internet banking” na huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimBanking.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Jina Namba ya Simu Barua Pepe
Tully Esther Mwambapa +255 769 200 600

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Godwin Semunyu +254 784 002 020 This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

(function($){ $(document).on('ready', function() { }); })(jQuery);